MalisaGJ's banner
MalisaGJ's profile picture

MalisaGJ

@MalisaGJ_45,038 subscribers

Award winning Philanthropist || SBC Specialist || Human Rights Activist || Simba SC Die Hard Fan

Shorts

Bwana Pasta akataka kutoka nje ya script akajikuta anagota "eeeh eeeh" kama guta lililofeli breki. Ila CCM wanajua kudhalilisha sana aisee. Ptuu mbaka 🤣🤣

Bwana Pasta akataka kutoka nje ya script akajikuta anagota "eeeh eeeh" kama guta lililofeli breki. Ila CCM wanajua kudhalilisha sana aisee. Ptuu mbaka 🤣🤣

65,439 views

Kwamba hujui kule kwako Mbeya yule kijana Shadrack Chaula aliyechoma picha ya Rais anadaiwa kutekwa na hadi leo hajulikani kama yupo hai au ameuawa? Hujasikia kijana Deus Soka na wenzake watatu wametekwa? Hujasikia miili ya watu iliyofukuliwa kwa Mganga huko Singida? Hujasikia dada aliyekatwa mapanga na viungo vyake kutawanywa maeneo mbalimbali jijini Dar? Hujasikia Polisi wameua mwananchi huko Lamadi, Simiyu baada ya wananchi kuandamana kufuatia matukio ya watoto kutekwa? Kwako haya sio mambo ya dharura? Ingekua Deus ni mwanao ametekwa na leo ni siku ya 9 hujui kama yuko hai au amekufa ungetoa majibu haya mepesi? Unadhani wazazi wake wanajisikiaje wakisikiliza haya majibu yako? Dada Tulia, hiki ukichokifanya kitakuhukumu wewe na kizazi chako mbele za Mungu aliye hai. Ni bora ungekaa kimya kuliko kusema hujui. Dalai Lama aliwahi kusema kama huwezi kumsaidia mtu angalau jitahidi usimuumize. Wewe umeshindwa kusaidia wanaodaiwa kutekwa, kupotea na kuuawa, lakini umetoa kauli ambayo inawaumiza ndugu na jamaa zao. Hamna shida. Mungu yupo.!

51,092 views

Huu sio mkutano wa siasa, ni wananchi wamevamia Kituo cha Polisi Lamadi wakidai Polisi wa eneo hilo wameshindwa kudhibiti matukio ya Watoto kutekwa na kupotea. Wananchi hao wamefunga barabara ya Mwanza-Simiyu-Mara kushinikiza Polisi kueleza watoto wao waliopotea wako wapi. Jeshi la Polisi limetumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya lakini wananchi hao wanaendelea kukabiliana nao.!

39,391 views

Videos

MalisaGJ_'s profile picture

"Nisaidieni naenda kuuawa, naenda kuuawa, siwajui hawa, naenda kuuawa" jamaa anapambania uhai wake nje ya Hotel ya Rovvenpec Resort iliyopo Kiluvya madukani, jijini Dar. Lakini wananchi wanashuhudia tu, na hawatoi msaada wowote. Yani ilitakiwa hicho kigari kigeuke "majivu" dakika sifuri lakini watu wanashangaa tu kama vile wanaangalia sinema. Angalau huyu aliyechukua video amesaidia kuhabarisha umma, lakini wengine wamesimama tu wakiangalia mwenzao akilalamika kwenda kuuawa. Halafu kesho maiti yake ikiokotwa huko Ununio watu haohao wangejifanya kusikitika. Watanzania wengi ni wanafiki sana aisee. Ptuu mbaka.! Ukifuatwa na hawa wahuni jitetee kwa nguvu zako zote, its a margin between death and life. Usitegemee watanzania maana wengi ni makondoo tu. Pigania uhai wako mwenyewe. Kama una silaha yoyote itumie kujihami. Usitembee kiboya. Huyu jamaa ubonge umemsaidia. Mungu kamjalia mwili na nguvu za kujitetea. Lakini angekua "kimbaumbau" kama mimi, saivi tungeshaandika BringBack za kutosha, au mwili wake ungeokotwa huko Ununio. Nimejisikia vibaya sana kuona vitendo vya utekaji vinafanyika katika nchi huru na viongozi wala hawajali. Fikiria "watekaji" wanaongea kwa kujiamini kwamba "ukigoma kuingia hapo tutakuua" na bado wananchi wanashangaa tu. Pamoja na jamaa kujitetea na kufanikiwa kuokoa roho yake, bado watekaji wamejibu kwa dharau kwamba "Tutakurudia" maana yake hajakwepa kifo. Amekiahirisha tu 😭. Halafu wale tuliowapa dhamana za uongozi wanatuambia kifo ni kifo tu. Mene mene tekeli na peresi. Mungu yupo.!

MalisaGJ

200,832 views • 1 year ago

MalisaGJ_'s profile picture

Add caption.! 😄😄

MalisaGJ

51,427 views • 10 months ago

MalisaGJ_'s profile picture

Baba kwa unyenyekevu mkubwa niseme nimesikitika kukusikiliza. Kwanza sikuamini kama ni wewe, maana hatujakuzoea hivi. Kwa miaka yote tangu ukiwa Mkuu wa Kanisa, umekua mtu imara, unayesimamia haki na usiyejihusisha na ushabiki wa kisiasa. Ulisimamia Kanisa vema na kutetea haki za watu katika nyakati ngumu za utawala wa awamu ya 5. Ni kweli awamu ya 6 ilianza vizuri tukashuhudia wafungwa wa kisiasa wakiachiwa huru, viongozi waliokimbia nchi wakikaribishwa kurudi, na mikutano ya kisiasa ikiruhusiwa. Kwahiyo ulikua na haki ya kumsifu Samia mwanzoni mwa utawala wake. Hata sisi tulisema mama anaupiga mwingi. Mimi ndiye mwasisi wa kauli hiyo. Lakini kwa sasa mambo yameharibika baba. Kuna matukio mengi yanayotishia haki na uhuru wa watu. Watu wanaripotiwa kutekwa na kupotea. Kipindi cha Magufuli ulisimama na kulaani vitendo hivyo, lakini kwa sasa hatujakusikia. Naomba nikukumbushe jirani yako hapo Kibosho Kindi, Deus Soka anadaiwa kutekwa pamoja marafiki zake wawili (Mbise na Mlay) maeneo ya Yombo Buza. Zaidi ya siku 70 sasa hawajulikani kama wapo hai au wameuawa. Hatujasikia ukikemea kama ulivyokemea awamu iliyopita. Lakini Deus na wenzake ni tone dogo la maji katika bahari iliyochafuka. TLS walitoa orodha ya watu 82 waliodaiwa kutekwa kwa mwaka huu. Yani kuanzia January hadi leo kuna roho 82 za watanzania wenzetu ziko mateka. Hivi hili halijakushtua Baba Askofu? Mbona hukulisemea? Yani watu 82 wanapotea kama kuku na Kanisa lipo kimya? Anyway tuseme hiyo list ya TLS hukuisikia. Je hata la mzee Kibao kushushwa kwenye basi na kwenda kuuawa kikatili hukusikia pia? Mbona hukukemea hata hilo? Halafu leo unasimama kupigia debe serikali hii iliyoshindwa kutuambia roho za watanzania wenzetu 82 zilipo? Serikali hii iliyoshindwa kuwakamata wauaji wa mzee Kibao, wakati walimchukua mchana kweupe? Serikali hii iliyoshindwa kuwakamata waliomteka Sativa. Baba kwa unyenyekevu nikuambie ukweli ambao wengi wataogopa kukuambia. Umetukosea watanzania, na umelikosea Kanisa. Kauli hizi zilipaswa kutolewa Katibu mwenezi wa CCM sio wewe. Umejenga heshima kubwa kwa miaka mingi. Kosa hili dogo linaweza kuharibu mengi mazuri uliyofanya nyuma. Jikosoe, Jirudi, Jisahihishe.!

MalisaGJ

56,688 views • 1 year ago