
MalisaGJ
@MalisaGJ_ • 45,038 subscribers
Award winning Philanthropist || SBC Specialist || Human Rights Activist || Simba SC Die Hard Fan
Shorts
Videos

"Nisaidieni naenda kuuawa, naenda kuuawa, siwajui hawa, naenda kuuawa" jamaa anapambania uhai wake nje ya Hotel ya Rovvenpec Resort iliyopo Kiluvya madukani, jijini Dar. Lakini wananchi wanashuhudia tu, na hawatoi msaada wowote. Yani ilitakiwa hicho kigari kigeuke "majivu" dakika sifuri lakini watu wanashangaa tu kama vile wanaangalia sinema. Angalau huyu aliyechukua video amesaidia kuhabarisha umma, lakini wengine wamesimama tu wakiangalia mwenzao akilalamika kwenda kuuawa. Halafu kesho maiti yake ikiokotwa huko Ununio watu haohao wangejifanya kusikitika. Watanzania wengi ni wanafiki sana aisee. Ptuu mbaka.! Ukifuatwa na hawa wahuni jitetee kwa nguvu zako zote, its a margin between death and life. Usitegemee watanzania maana wengi ni makondoo tu. Pigania uhai wako mwenyewe. Kama una silaha yoyote itumie kujihami. Usitembee kiboya. Huyu jamaa ubonge umemsaidia. Mungu kamjalia mwili na nguvu za kujitetea. Lakini angekua "kimbaumbau" kama mimi, saivi tungeshaandika BringBack za kutosha, au mwili wake ungeokotwa huko Ununio. Nimejisikia vibaya sana kuona vitendo vya utekaji vinafanyika katika nchi huru na viongozi wala hawajali. Fikiria "watekaji" wanaongea kwa kujiamini kwamba "ukigoma kuingia hapo tutakuua" na bado wananchi wanashangaa tu. Pamoja na jamaa kujitetea na kufanikiwa kuokoa roho yake, bado watekaji wamejibu kwa dharau kwamba "Tutakurudia" maana yake hajakwepa kifo. Amekiahirisha tu 😭. Halafu wale tuliowapa dhamana za uongozi wanatuambia kifo ni kifo tu. Mene mene tekeli na peresi. Mungu yupo.!
MalisaGJ200,832 views • 1 year ago

Kuna watu watatu wasioweza kushaurika wala kubadilika kirahisi; 1. Mwanaume mwenye pesa (hasa aliyepata pesa ghafla). 2. Mwanamke aliyezama penzini (hasa penzi la kwanza). 3. Mwanamke wa kiafrika anayemuamini Mtume/Nabii wake. Hao watu watatu hata uwafunge jela hawashauriki. Hasa huyo wa 3 ndio balaa. Yupo tayari ndoa ivunjike, apoteze familia, na hata ikibidi kufa kuliko umkosoe Mtume/Nabii wake 🤣🙌🏻. Subhanallah.!
MalisaGJ115,653 views • 2 years ago

Naomba asitekwe tafadhali. Sikilizeni ujumbe, ukiwauma kunyweni maji mengi mjikaze.!
MalisaGJ92,916 views • 1 year ago

Ngoja niulize swali huenda mimi ndo sijaelewa. Huyu Mwenyekiti wa kitongoji amelalamika kuhusu hofu yake ya kutekwa au kuuawa na DC. Sasa kwanini Mwigulu amemwelekeza tena DC huyohuyo kumlinda? DC ambaye ni mtuhumiwa anawezaje kumlinda mtu aliyeenda kumshtaki kwa boss wake? 🤷♂️🤷♂️
MalisaGJ27,394 views • 6 months ago

Kada maarufu wa Chadema mkoani Tanga, Kombo Mbwana maarufu kama "Mzalendo" anadaiwa kutekwa Tarehe 16/06/2024 majira ya saa 2 mbili 2 asubuhi, akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Kwamatuku Wilaya Ya Handeni. Mke wa Kombo anasema siku ya tukio, walipata mgeni aliyejitambulisha kuwa ni "mtu wa serikali" akamtaka Kombo waongee, akieleza kwamba kuna eneo alinunua karibu na alipojenga Kombo. Baada ya kutoka Kombo hakurudi na hakupatikana tena kwenye simu hadi leo. Na huo ndio ulikua mwisho wa Kombo kuonekana hadharani. Hadi leo hajulikani alipo. Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Chadema mkoa wa Tanga, ndugu Michael Haule inaeleza kuwa wamemtafuta Kombo katika vituo vya Polisi na hospitalini lakini hawajamuona. Wametoa taarifa polisi lakini Kamanda wa Polisi amesema nao pia wanamtafuta. #JusticeForKombo #BringBackKombo
MalisaGJ72,588 views • 2 years ago

Kauli ya Baba, Rev.Dr.Charles Kitima (PhD), Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu nchini (TEC). Hakikisha unashirikisha "medula oblangata" ili kumuelewa vizuri. Kama hukupata chanjo ya pepopunda utotoni rudia kusikiliza mara 3 vinginevyo hutamuelewa. Roma locuta, causa finita est.!
MalisaGJ49,853 views • 1 year ago

Dakika 3 za dhahabu za Askofu Jacob Mameo Ole Paulo, Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Morogoro. Sikiliza neno kwa neno, tena kwa utulivu. Anatema madini ambayo si rahisi kuyapata kwa viongozi wengine wa dini. Hakika hili ndio NENO KUU la IJUMAA KUU ya mwaka huu. Viongozi wakuu wa serikali waione hii clip kwenye jalada.!
MalisaGJ47,837 views • 1 year ago

Baba kwa unyenyekevu mkubwa niseme nimesikitika kukusikiliza. Kwanza sikuamini kama ni wewe, maana hatujakuzoea hivi. Kwa miaka yote tangu ukiwa Mkuu wa Kanisa, umekua mtu imara, unayesimamia haki na usiyejihusisha na ushabiki wa kisiasa. Ulisimamia Kanisa vema na kutetea haki za watu katika nyakati ngumu za utawala wa awamu ya 5. Ni kweli awamu ya 6 ilianza vizuri tukashuhudia wafungwa wa kisiasa wakiachiwa huru, viongozi waliokimbia nchi wakikaribishwa kurudi, na mikutano ya kisiasa ikiruhusiwa. Kwahiyo ulikua na haki ya kumsifu Samia mwanzoni mwa utawala wake. Hata sisi tulisema mama anaupiga mwingi. Mimi ndiye mwasisi wa kauli hiyo. Lakini kwa sasa mambo yameharibika baba. Kuna matukio mengi yanayotishia haki na uhuru wa watu. Watu wanaripotiwa kutekwa na kupotea. Kipindi cha Magufuli ulisimama na kulaani vitendo hivyo, lakini kwa sasa hatujakusikia. Naomba nikukumbushe jirani yako hapo Kibosho Kindi, Deus Soka anadaiwa kutekwa pamoja marafiki zake wawili (Mbise na Mlay) maeneo ya Yombo Buza. Zaidi ya siku 70 sasa hawajulikani kama wapo hai au wameuawa. Hatujasikia ukikemea kama ulivyokemea awamu iliyopita. Lakini Deus na wenzake ni tone dogo la maji katika bahari iliyochafuka. TLS walitoa orodha ya watu 82 waliodaiwa kutekwa kwa mwaka huu. Yani kuanzia January hadi leo kuna roho 82 za watanzania wenzetu ziko mateka. Hivi hili halijakushtua Baba Askofu? Mbona hukulisemea? Yani watu 82 wanapotea kama kuku na Kanisa lipo kimya? Anyway tuseme hiyo list ya TLS hukuisikia. Je hata la mzee Kibao kushushwa kwenye basi na kwenda kuuawa kikatili hukusikia pia? Mbona hukukemea hata hilo? Halafu leo unasimama kupigia debe serikali hii iliyoshindwa kutuambia roho za watanzania wenzetu 82 zilipo? Serikali hii iliyoshindwa kuwakamata wauaji wa mzee Kibao, wakati walimchukua mchana kweupe? Serikali hii iliyoshindwa kuwakamata waliomteka Sativa. Baba kwa unyenyekevu nikuambie ukweli ambao wengi wataogopa kukuambia. Umetukosea watanzania, na umelikosea Kanisa. Kauli hizi zilipaswa kutolewa Katibu mwenezi wa CCM sio wewe. Umejenga heshima kubwa kwa miaka mingi. Kosa hili dogo linaweza kuharibu mengi mazuri uliyofanya nyuma. Jikosoe, Jirudi, Jisahihishe.!
MalisaGJ56,688 views • 1 year ago

Watu waliojitambulisha kuwa ni Askari Polisi wakivamia ofisi za Taasisi ya #ReachOutTanzania zilizopo eneo la Makumbusho jijini DSM, wakimtafuta Mwanasheria wa taasisi hiyo Ndugu Adv.Alphonce Lusako. Inaelezwa watu hao walikuja katika kundi kubwa ambapo wenye mitutu ya bunduki walibaki nje kwenye gari (hawaonekani kwenye CCTV), na wawili wenye bastola waliingia ndani kumsaka Lusako, kama walivyonaswa kwenye camera.!
MalisaGJ52,816 views • 1 year ago

Polisi wametumia risasi za moto kutawanya wananchi walioandamana kupinga matukio ya watoto wao kupotea eneo la Lamadi, wilayani Busega mkoani Simiyu. Wananchi hao wamewalaumu Polisi kwa kutochukua hatua za kuridhisha kukabiliana na vitendo vya watoto wao kupotea. Katika makabiliano ya Polisi na raia leo, inadaiwa watu kadhaa wamejeruhiwa na wengine wakihisiwa kufariki. Inaelezwa kuwa wanaojeruhiwa wanapelekwa hospitalini lakini wanaofariki wananchi wanawachukua na kuwapeleka kituo cha Polisi kuhoji kwanini wameuawa bila hatia? #ONYO: Maudhui ya video hii yanaweza kuumiza hisia, hivyo kama unafadhaishwa na majeraha ya damu tafadhali usifungue.!
MalisaGJ53,989 views • 2 years ago