
MalisaGJ
@MalisaGJ_ • 44,817 subscribers
Award winning Philanthropist || SBC Specialist || Human Rights Activist || Simba SC Die Hard Fan
Shorts
Videos

"Nisaidieni naenda kuuawa, naenda kuuawa, siwajui hawa, naenda kuuawa" jamaa anapambania uhai wake nje ya Hotel ya Rovvenpec Resort iliyopo Kiluvya madukani, jijini Dar. Lakini wananchi wanashuhudia tu, na hawatoi msaada wowote. Yani ilitakiwa hicho kigari kigeuke "majivu" dakika sifuri lakini watu wanashangaa tu kama vile wanaangalia sinema. Angalau huyu aliyechukua video amesaidia kuhabarisha umma, lakini wengine wamesimama tu wakiangalia mwenzao akilalamika kwenda kuuawa. Halafu kesho maiti yake ikiokotwa huko Ununio watu haohao wangejifanya kusikitika. Watanzania wengi ni wanafiki sana aisee. Ptuu mbaka.! Ukifuatwa na hawa wahuni jitetee kwa nguvu zako zote, its a margin between death and life. Usitegemee watanzania maana wengi ni makondoo tu. Pigania uhai wako mwenyewe. Kama una silaha yoyote itumie kujihami. Usitembee kiboya. Huyu jamaa ubonge umemsaidia. Mungu kamjalia mwili na nguvu za kujitetea. Lakini angekua "kimbaumbau" kama mimi, saivi tungeshaandika BringBack za kutosha, au mwili wake ungeokotwa huko Ununio. Nimejisikia vibaya sana kuona vitendo vya utekaji vinafanyika katika nchi huru na viongozi wala hawajali. Fikiria "watekaji" wanaongea kwa kujiamini kwamba "ukigoma kuingia hapo tutakuua" na bado wananchi wanashangaa tu. Pamoja na jamaa kujitetea na kufanikiwa kuokoa roho yake, bado watekaji wamejibu kwa dharau kwamba "Tutakurudia" maana yake hajakwepa kifo. Amekiahirisha tu 😭. Halafu wale tuliowapa dhamana za uongozi wanatuambia kifo ni kifo tu. Mene mene tekeli na peresi. Mungu yupo.!
MalisaGJ200,439 görüntüleme • 1 yıl önce

Kuna watu watatu wasioweza kushaurika wala kubadilika kirahisi; 1. Mwanaume mwenye pesa (hasa aliyepata pesa ghafla). 2. Mwanamke aliyezama penzini (hasa penzi la kwanza). 3. Mwanamke wa kiafrika anayemuamini Mtume/Nabii wake. Hao watu watatu hata uwafunge jela hawashauriki. Hasa huyo wa 3 ndio balaa. Yupo tayari ndoa ivunjike, apoteze familia, na hata ikibidi kufa kuliko umkosoe Mtume/Nabii wake 🤣🙌🏻. Subhanallah.!
MalisaGJ115,639 görüntüleme • 1 yıl önce

Ngoja niulize swali huenda mimi ndo sijaelewa. Huyu Mwenyekiti wa kitongoji amelalamika kuhusu hofu yake ya kutekwa au kuuawa na DC. Sasa kwanini Mwigulu amemwelekeza tena DC huyohuyo kumlinda? DC ambaye ni mtuhumiwa anawezaje kumlinda mtu aliyeenda kumshtaki kwa boss wake? 🤷♂️🤷♂️
MalisaGJ27,378 görüntüleme • 3 ay önce

Naomba asitekwe tafadhali. Sikilizeni ujumbe, ukiwauma kunyweni maji mengi mjikaze.!
MalisaGJ92,899 görüntüleme • 1 yıl önce

Asante sana Baba Askofu Malasusa. Hii ni comeback ya nguvu kabisa. Dakika za jioooni Mkuu wa Kanisa anaipa ushindi timu ya HAKI. Asante Baba. Kauli yako ndio kauli rasmi ya Kanisa. Kanisa halitampigia debe mtu kwa chama chake, dini yake, jinsia yake, sura yake wala kabila lake. Awe Msukuma au Mpare its not a church business. Awe na macho ya kurembua au makavu kama ya Kabudi its neither your trade. Kanisa litasimama upande wa HAKI, UZALENDO na UADILIFU. Kanisa litafundisha watu wachaguliwe kwa sifa zao, sio jinsia zao, vyama vyao, au dini zao. Huu ndio msimamo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, lenye waumini takribani milioni 10. Kanisa la pili kwa ukubwa nchini baada ya Kanisa takatifu Katoliki la Mitume, na Kanisa la pili kwa ukubwa kwenye fungamano la Makanisa ya Kilutheri duniani baada ya Kanisa la Udachi (Ujerumani). Sasa kwa kuwa Mkuu wa Kanisa ameshatoa msimamo wa Kanisa, basi tuishi humo. Mdogo akikosea, mkubwa akasawazisha, busara inatufundisha kusahau makosa na kusimama kwenye masahihisho. Ndugu yangu #NIPENI_MAUA_YANGU💐 aliwahi kuimba "Nitasimama imara kama KKKT." Uimara wa KKKT ni katika misingi ya Kanisa ambayo ni "Sola 4" yani Sola Christus, Sola Scriptura, Sola Fide, Sola Gratia" (Kristo tu, Neno tu, Imani tu, Neema tu). Tuishi humo.!
MalisaGJ81,790 görüntüleme • 1 yıl önce

Kauli ya Baba, Rev.Dr.Charles Kitima (PhD), Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu nchini (TEC). Hakikisha unashirikisha "medula oblangata" ili kumuelewa vizuri. Kama hukupata chanjo ya pepopunda utotoni rudia kusikiliza mara 3 vinginevyo hutamuelewa. Roma locuta, causa finita est.!
MalisaGJ49,479 görüntüleme • 1 yıl önce

Dakika 3 za dhahabu za Askofu Jacob Mameo Ole Paulo, Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Morogoro. Sikiliza neno kwa neno, tena kwa utulivu. Anatema madini ambayo si rahisi kuyapata kwa viongozi wengine wa dini. Hakika hili ndio NENO KUU la IJUMAA KUU ya mwaka huu. Viongozi wakuu wa serikali waione hii clip kwenye jalada.!
MalisaGJ47,795 görüntüleme • 1 yıl önce
1:48
Sensitive content
This media may contain sensitive content.

Baba kwa unyenyekevu mkubwa niseme nimesikitika kukusikiliza. Kwanza sikuamini kama ni wewe, maana hatujakuzoea hivi. Kwa miaka yote tangu ukiwa Mkuu wa Kanisa, umekua mtu imara, unayesimamia haki na usiyejihusisha na ushabiki wa kisiasa. Ulisimamia Kanisa vema na kutetea haki za watu katika nyakati ngumu za utawala wa awamu ya 5. Ni kweli awamu ya 6 ilianza vizuri tukashuhudia wafungwa wa kisiasa wakiachiwa huru, viongozi waliokimbia nchi wakikaribishwa kurudi, na mikutano ya kisiasa ikiruhusiwa. Kwahiyo ulikua na haki ya kumsifu Samia mwanzoni mwa utawala wake. Hata sisi tulisema mama anaupiga mwingi. Mimi ndiye mwasisi wa kauli hiyo. Lakini kwa sasa mambo yameharibika baba. Kuna matukio mengi yanayotishia haki na uhuru wa watu. Watu wanaripotiwa kutekwa na kupotea. Kipindi cha Magufuli ulisimama na kulaani vitendo hivyo, lakini kwa sasa hatujakusikia. Naomba nikukumbushe jirani yako hapo Kibosho Kindi, Deus Soka anadaiwa kutekwa pamoja marafiki zake wawili (Mbise na Mlay) maeneo ya Yombo Buza. Zaidi ya siku 70 sasa hawajulikani kama wapo hai au wameuawa. Hatujasikia ukikemea kama ulivyokemea awamu iliyopita. Lakini Deus na wenzake ni tone dogo la maji katika bahari iliyochafuka. TLS walitoa orodha ya watu 82 waliodaiwa kutekwa kwa mwaka huu. Yani kuanzia January hadi leo kuna roho 82 za watanzania wenzetu ziko mateka. Hivi hili halijakushtua Baba Askofu? Mbona hukulisemea? Yani watu 82 wanapotea kama kuku na Kanisa lipo kimya? Anyway tuseme hiyo list ya TLS hukuisikia. Je hata la mzee Kibao kushushwa kwenye basi na kwenda kuuawa kikatili hukusikia pia? Mbona hukukemea hata hilo? Halafu leo unasimama kupigia debe serikali hii iliyoshindwa kutuambia roho za watanzania wenzetu 82 zilipo? Serikali hii iliyoshindwa kuwakamata wauaji wa mzee Kibao, wakati walimchukua mchana kweupe? Serikali hii iliyoshindwa kuwakamata waliomteka Sativa. Baba kwa unyenyekevu nikuambie ukweli ambao wengi wataogopa kukuambia. Umetukosea watanzania, na umelikosea Kanisa. Kauli hizi zilipaswa kutolewa Katibu mwenezi wa CCM sio wewe. Umejenga heshima kubwa kwa miaka mingi. Kosa hili dogo linaweza kuharibu mengi mazuri uliyofanya nyuma. Jikosoe, Jirudi, Jisahihishe.!
MalisaGJ56,642 görüntüleme • 1 yıl önce

Watu waliojitambulisha kuwa ni Askari Polisi wakivamia ofisi za Taasisi ya #ReachOutTanzania zilizopo eneo la Makumbusho jijini DSM, wakimtafuta Mwanasheria wa taasisi hiyo Ndugu Alphonce Lusako. Inaelezwa watu hao walikuja katika kundi kubwa ambapo wenye mitutu ya bunduki walibaki nje kwenye gari (hawaonekani kwenye CCTV), na wawili wenye bastola waliingia ndani kumsaka Lusako, kama walivyonaswa kwenye camera.!
MalisaGJ52,800 görüntüleme • 1 yıl önce

Polisi wametumia risasi za moto kutawanya wananchi walioandamana kupinga matukio ya watoto wao kupotea eneo la Lamadi, wilayani Busega mkoani Simiyu. Wananchi hao wamewalaumu Polisi kwa kutochukua hatua za kuridhisha kukabiliana na vitendo vya watoto wao kupotea. Katika makabiliano ya Polisi na raia leo, inadaiwa watu kadhaa wamejeruhiwa na wengine wakihisiwa kufariki. Inaelezwa kuwa wanaojeruhiwa wanapelekwa hospitalini lakini wanaofariki wananchi wanawachukua na kuwapeleka kituo cha Polisi kuhoji kwanini wameuawa bila hatia? #ONYO: Maudhui ya video hii yanaweza kuumiza hisia, hivyo kama unafadhaishwa na majeraha ya damu tafadhali usifungue.!
MalisaGJ53,853 görüntüleme • 1 yıl önce

Kwa akili ndogo kama hizi napata mashaka anaongozaje watu "wajanja" kama wa Arusha; 1. Kwanza hajui wajibu wake kama Mbunge. Anauliza vikao gani. Hajui kwamba yeye ni mjumbe wa Kamati ya maendeleo ya mkoa (RCC) na Mkuu wa Mkoa ndiye mwenyekiti wake? Hajui kwamba yeye ni mjumbe wa Bodi ya barabara ya mkoa na RC ndiye mwenyekiti wake? Hajui kwamba yeye ni mjumbe wa vikao vya Halmashauri? Yani anadhani vikao vya mbunge vinaishia bungeni na kwenye kamati? Hopeless kabisa.! 2. Pili Mrisho ni "arrogant" sana. Eti mimi sio afisa tarafa wala mtendaji wa kata? Hii kauli ina maana gani? Kwamba maafisa tarafa na watendaji wa kata sio level yako? Kwamba u are better than them? Usichojua ni kwamba wapo maafisa tarafa wamekuzidi akili, maarifa na hekima, ila tu hawajapata bahati ya kuwa ulipo. Ipo siku hao maafisa tarafa unaowazodoa wanaweza kuwa mawaziri na wewe ukakosa hata ubunge. Biblia inasema wakati na bahati huwapata wote (Mhubiri 9:11). Be humble.! 3. Hoja ya Makonda ni kwamba wewe kama mbunge una nafasi ya kushiriki vikao vya kupanga maendeleo ya jimbo lako badala ya kusubiri wengine wapange halafu uje kujiliza hadharani. Kwa mfano ungehudhuria vikao vya road fund ungejua serikali imetenga kiasi gani kwa ujenzi wa barabara za mkoa wa Arusha. Ungejua jimbo lako limepewa kilomita ngapi. Ungejua TARURA wamejipangaje kwenye barabara za mitaa. Lakini kama hushiriki vikao unasubiri Waziri afike ndipo uongee hadharani, huko ni kutafuta cheap popularity. Badilika.! 4. Unaposema vikao vyako ni vya bunge na RC hawezi kuingia ni kutafuta "utukufu" ambao huna. Wewe ni mwakilishi wa wananchi, lakini unapokua jimboni unakua chini ya mamlaka ya mkoa. Ndio maana kwenye RCC unaingia kama mjumbe lakini Mwenyekiti wako ni RC kwa sababu yeye ndio Commanding Officer wa mkoa. Vikao vya Halmashauri unaingia kama Diwani, lakini RC akija anakua overseer. Kwahiyo acha kujivika utukufu hewa.! 5. Ulipokua RC ulijaribu kumdiscredit Lema na kuonesha Mbunge hana mchango wowote kwenye maendeleo. Uliwahi kumdhalilisha Lema hadharani na kumwambia ajifunze kuheshimu mamlaka. Hukujua kama dunia inazunguka? Sasa na wewe jifunze kuheshimu Mamlaka. Mwaka huu umekopa kausha damu, kaa kwa kutulia.!
MalisaGJ38,476 görüntüleme • 1 yıl önce