
Gerson Msigwa
@MsigwaGerson • 849,969 subscribers
The Permanent Secretary of Information, Culture, Arts and Sports || Chief Government Spokesperson of Tanzania.
Videos

Ndugu zangu Waandishi wa Habari mnaonipigia simu nyingi na kunitumia ujumbe mkiniuliza kuhusu jambo hili, ni hivi; Hili lilikuwa wasilisho langu katika kikao kazi cha Maafisa Habari nililotoa tarehe 8 Mei, 2026 Mjini Njombe nikiwa msimamizi na mratibu wasilisho langu katika vitengo cya habari Serikalini (sikiliza video mpaka mwisho) Nilikuwa nikitekeleza wajibu wangu na niliyoyazungumza/niliyoyakumbusha ni kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa, Sheria ya Utumishi wa Umma na Kanuni za Utumishi wa Umma. Naamini mmenielewa, kazi njema. #SinaNoma
Gerson Msigwa89,997 views • 2 months ago

Kuna wakati ni vizuri kuwasikiliza watumiaji wenyewe wa Bandari. Asante Mnyalukolo CHRIS LUKOSI NB. Bandari haijauzwa, haitauzwa na hakuna mpango wa kuiuza. Juhudi zinazofanyika ni za kuongeza ufanisi wa bandari kwa kuweka uwekezaji mkubwa kupitia sekta binafsi ambao utatuongezea mapato kwa zaidi ya mara 3 ikilinganishwa na sasa, utatuongezea ajira, utavutia biashara ya bandari yetu, utatuongezea manufaa ya reli yetu ya kisasa (SGR) na utatujengea uwezo wa kuendesha bandari kisasa. 🙏🏼🙏🏼 GlobalNetTVChannel
Gerson Msigwa568,085 views • 3 years ago

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI TANZANIA. #UsishirikiUhalifu
Gerson Msigwa41,984 views • 2 months ago

HATIMAYE meli yetu kongwe na ya kihistoria MV Liemba imeanza majaribio ikiwa ni maandalizi ya kuanza kazi rasmi ifikapo tarehe 01 Septemba, 2026 baada ya kusimama kwa takribani miaka 10 kutokana na kuhitaji ukarabati mkubwa. Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kutafuna fupa gumu la kukarabati meli ili kuirejesha katika uhai mpya wa matumizi ya miaka 50. Kwa wasiojua meli hii ina umri wa miaka 113. Ilijengwa kwa mara ya kwanza nchini Ujerumani mwaka 1913 na Meyer Werft wa Papenburg, ikapewa jina la Graf von Goetzen ambaye alikuwa Gavana wa Kijerumani Afrika Mashariki. Kati ya mwaka 1914-1915 ilibomolewa katika vipande 5,000 ambavyo vilisafirishwa kwa meli mpaka Bandari ya Dar es Salaam na kisha kusafirishwa kwa treni kupitia reli ya kati (MGR) hadi katika fukwe za Ziwa Tanganyika Mkoani Kigoma ambako iliunganishwa upya kwa ajili ya kutumika katika Ziwa Tanganyika kusafirisha watu na mizigo. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Ujerumani ilitawala Ziwa Tanganyika lakini kutokana na tishio kubwa la majeshi ya Wabelgiji na Waingereza, wafanyakazi Wajerumani wa meli hiyo waliamua kuizamisha majini katika Bandari ya Katabe ili kuificha isichukuliwe lakini kabla ya kuizamisha walipaka grisi katika injini yake yote ili isiharibiwe na maji. Hata hivyo, mwaka 1924 timu uokozi ya majeshi ya wanamaji wa Uingereza baada ya kukamata utawala iliibua meli hiyo kutoka katika sakafu ya Ziwa Tanganyika na mwaka 1927 Waingereza walifanikiwa kuirejesha katika matumizi ikisafirisha watu na mizigo. Wakati huo ndipo wakaibadilishwa jina na kuiita MV Liemba (Liemba ni neno la kabila la Kirungu likiwa na maana ziwa) Tangu wakati huo meli hii imekuwa katika matumizi mpaka mwaka 2016 ilipokuwa katika hali mbaya zaidi na hatimaye kusimamishwa kutokana na kuhitaji matengenezo makubwa. Serikali imefanya ukabari wa kufunga kila kitu kipya na cha kisasa. Sasa meli ina uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 200 za mizigo ikiwa na kasi zaidi na mifumo yote mipya. Itatumika kuhudumia Tanzania, Zambia, Burundi na Kongo. Kwa ufupi tuna meli kwa biashara, usafiri wa watu na utalii. (Mzee NONGWA ole wako useme hili nalo halina maana🤣🤣)
Gerson Msigwa14,394 views • 28 days ago

U F A F A N U Z I. 1. Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) lipo katika mchakato wa kuanza safari za Ulaya. Huko sio kuzuiwa. 2. Serikali haijanunua na haina mpango wa kuanza kununua vichwa vya treni za SGR vya kutumia mafuta ya dizeli. Tunanunua vya umeme, haturudi nyuma. PUUZENI UPOTOSHAJI HUU.
Gerson Msigwa111,732 views • 1 year ago

Hii hapa habari njema kwa Watumishi wa Umma. Ni nyongeza ya kima cha chini cha mshahara kwa asilimia 35.1. Kima cha chini kitaongezeka kutoka shilingi 370,000/- hadi shilingi 500,000/-. Pia nyongeza nono kwa watumishi wa ngazi nyingine za mshahara. Nikisema KAZI NA UTU!!!! unajibu………. Asante Mheshimiwa Rais. Hii ni imani kubwa kwa Watumishi wa Umma na imani huzaa imani (wenye D mbili tumekusoma) #KaziIendelee
Gerson Msigwa78,531 views • 1 year ago

HILI HAPA JINGINE KUBWA KWA TANZANIA. Ni mkutano mkubwa unaowakutanisha Wakuu wa Nchi za Afrika, viongozi mbalimbali, Wataalamu, sekta binafsi, kampuni na taasisi za maendeleo na taasisi za fedha watakaokuja Dar es Salaam tarehe 5-6 Agosti, 2026 kuhudhuria mkutano mkubwa wa kiuchumi uitwao Afrika50 (Africa50). Tazama makala hii fupi kwa ajili ya uelewa wa mkutano na fursa zake. #KaziIendelee
Gerson Msigwa10,820 views • 1 month ago

SERIKALI SIKIVU IMEWASIKILIZA WAHESHIMIWA WABUNGE KUHUSU BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA 2026/27, IMEKUBALI KUFANYA MAREKEBISHO KWA KUWEKA MBELE MASLAHI YA WANANCHI. Shukrani nyingi kwa Kiongozi Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuijali Tanzania na kuwajali Watanzania. // Msikilize Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azan Zungu akitimisha uwasilishaji wa muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2026 baada ya Bunge zima kupitisha kura ya NDIO. #KaziIendelee
Gerson Msigwa17,743 views • 2 months ago