正在加载视频...

视频加载失败

10,973 次观看 • 5 个月前 •via X (Twitter)

0 条评论

暂无评论

原始帖子的评论将显示在这里

相关视频

VIDEO: Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Askofu Dkt. Benson Bagonza, amesema kwa sasa yanahitajika maridhiano ya kweli ili kulirudisha taifa katika amani na umoja wa kweli, huku akionya kwamba "taifa haliwezi kuongozwa kwa ujanjaujanja". Bagonza ameeleza hayo Desemba 21, 2025 katika ibada ya ubarikio wa wachungaji Dayosisi ya Karagwe, Usharika wa Lukajange- Kanisa Kuu ambapo huo ulikuwa ni ujumbe alioutoa kwa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene aliyehudhuria ibada hiyo kama mgeni rasmi. "Kimsingi, yanahitajika maridhiano ya kweli ili kurejesha amani na umoja wa taifa letu. Hakuna anayenufaika na mgawanyiko unaoendelea- wote ni wahanga na tunahitaji umoja na mshikamano wetu kama tulivyokuwa tukiishi. Katika mchakato mzima wa maridhiano, tujiepushe na sumu 5 zinazoishi...Baba wa Taifa aliwahi kuonya kuwa, Taifa haliwezi kuongozwa kiujanja ujanja"amesema Bagonza. Bagonza amesema katika mchakato mzima wa maridhiano mambo mbalimbali yanapaswa kuepukwa ikiwamo hila, kutafuta ushindi, kukwepa ukweli, matumizi ya madaraka na kujinufaisha na maridhiano. Ameongeza kwamba mijadala inayojadili "kipi ni bora kati ya haki na amani" si ya muhimu kutokana na alichosema katika mijadala hiyo kila mmoja anaonekana ni mshindi. "Mgeni wetu maalum naelewa kwa sasa mna mambo mengi sana mnayoshughulika nayo, mimi ninaloliona na la muhimu juu ya yote ni maridhiano ya kweli. Ile mijadala yetu ya kila siku juu ya kipi ni bora kati ya haki na amani kwa sasa si muhimu sana, kila mmoja ni mshindi anayependa haki ni mshindi na anayependa amani ni mshindi”, amesema. Hata hivyo amebainisha kwamba, ili kuirejesha nchi katika hali iliyozoeleka, zipo gharama za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisera ambazo kama nchi "tutatakiwa kuzikubali".

Jambo TV

10,699 次观看 • 7 个月前

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 225 Mhe. Lissu anaendelea hapa. Kama mtakumbuka nilisema ninavyoishi Ukonga, siruhusiwi kuonana na Mawakili wangu in private. Mnaruhusiwa kutembelea Magereza naomba mliangalie na hili kama itawapendeza inawapa Mamlaka ya kutoa mapendekezo na mamlaka za Magereza kurekebisha masuala yanayohusu wafungwa kama haya niliyosema. Ni muhimu kwamba kuwasiliana na washauri wangu wa kisheria ilindwe kama sheria inavyosema bila kusikilizwa na maafisa wa Magereza. Ni hayo tu Waheshimiwa Mhe. Tundu Lissu amemaliza na amekaa sasa. Majaji wanaandika hapa. Anasimama Renatus Mkude kuwa tutampatia hizi nyaraka ndani ya siku 14 tutampatia. Hili la masuala ya utawala wa mambo ya magereza kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha National Prosecution Act na sisi ofisi ya DPP tutatembelea ili kuhakisha kunakuwa na fair trial. Wameombwa Majaji anasema DPP ataenda eti huko Magereza kuangalia haki za Mtuhumiwa. Uongo uongo uongo. Hawana hata aibu hawa jamaa. Majaji wanaandika baada ya kusikia hayo kutoka kwa Wakili wa Serikali, Renatus Mkude. Majaji wanajadili pale. Yuko Jaji muda wote yeye huwa anacheka anafurahi tu sijui huwa anatabasamu jambo gani? Wanaofika hapa Mahakamani wanamfahamu vizuri. Jaji Ndunguru: Tumesikia hoja za Jamhuri na Hoja za Mshitakiwa nae kama ambavyo mshitakiwa ameturahisishia kuwa mikono yetu imefungwa kwamba yapo hayo maombi ya marejeo Mahakama ya Rufani. Sasa shauri hili linasimama hadi pale Mahakama ya Rufani itakapotoa uamuzi. Suala la Gerezani wakili wa Serikali amesema na sisi pia tumelichukua. Mwenendo wa shauri hili unasimama hadi pale mambo ya Court of Appeal yatakapoisha. So kesi hii imeahirishwa hadi hapo itakapoitwa tena. Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.

Twaha Mwaipaya

13,061 次观看 • 5 个月前