Video wird geladen...

Video konnte nicht geladen werden

Zur Startseite

10,994 Aufrufe • vor 7 Monaten •via X (Twitter)

0 Kommentare

Keine Kommentare verfügbar

Kommentare vom Original-Post werden hier angezeigt

Ähnliche Videos

VIDEO: Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Askofu Dkt. Benson Bagonza, amesema kwa sasa yanahitajika maridhiano ya kweli ili kulirudisha taifa katika amani na umoja wa kweli, huku akionya kwamba "taifa haliwezi kuongozwa kwa ujanjaujanja". Bagonza ameeleza hayo Desemba 21, 2025 katika ibada ya ubarikio wa wachungaji Dayosisi ya Karagwe, Usharika wa Lukajange- Kanisa Kuu ambapo huo ulikuwa ni ujumbe alioutoa kwa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene aliyehudhuria ibada hiyo kama mgeni rasmi. "Kimsingi, yanahitajika maridhiano ya kweli ili kurejesha amani na umoja wa taifa letu. Hakuna anayenufaika na mgawanyiko unaoendelea- wote ni wahanga na tunahitaji umoja na mshikamano wetu kama tulivyokuwa tukiishi. Katika mchakato mzima wa maridhiano, tujiepushe na sumu 5 zinazoishi...Baba wa Taifa aliwahi kuonya kuwa, Taifa haliwezi kuongozwa kiujanja ujanja"amesema Bagonza. Bagonza amesema katika mchakato mzima wa maridhiano mambo mbalimbali yanapaswa kuepukwa ikiwamo hila, kutafuta ushindi, kukwepa ukweli, matumizi ya madaraka na kujinufaisha na maridhiano. Ameongeza kwamba mijadala inayojadili "kipi ni bora kati ya haki na amani" si ya muhimu kutokana na alichosema katika mijadala hiyo kila mmoja anaonekana ni mshindi. "Mgeni wetu maalum naelewa kwa sasa mna mambo mengi sana mnayoshughulika nayo, mimi ninaloliona na la muhimu juu ya yote ni maridhiano ya kweli. Ile mijadala yetu ya kila siku juu ya kipi ni bora kati ya haki na amani kwa sasa si muhimu sana, kila mmoja ni mshindi anayependa haki ni mshindi na anayependa amani ni mshindi”, amesema. Hata hivyo amebainisha kwamba, ili kuirejesha nchi katika hali iliyozoeleka, zipo gharama za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisera ambazo kama nchi "tutatakiwa kuzikubali".

Jambo TV

10,702 Aufrufe • vor 9 Monaten