
Boniface Jacob
@ExMayorUbungo • 582,626 subscribers
Ex-mayor @Ubungo Municipal Council 2016-2020 Exmayor @Kinondoni Municipal council 2016 Jan to Nov. Ubungo councilor 2010-2020 BAEd Udsm CHADEMA CC MEMBER
Shorts
Videos

CHEKI MTU ALIVYONUSURIKA KUTEKWA ..! Tukio hili la Jaribio la utekaji limetokea katika Hotel ya Rovvenpec Resort iliyopo Kiluvya,Madukani Dar es Salaam. Jamaa aliiga mbinu zangu (Golden folk style) za kutumia nguvu na kugomea kuondoka nao hivyo kutokana na nguvu za jamaa na kelele zake za "naenda Kuuwawa" akafanikiwa kutetea uhai wake. Watekaji walishindwa kumbeba jamaa kama walivyo tarajia,na wakati wote huo hakuna mtu aliejitokeza kutoa msaada au Kuwahoji watekaji kwa lolote zaidi ya Kusimama na Kushuhudia.Inasikitisha sana. N.B 1.Somo la kujifunza ni kuwa Kuna mstari mwembamba sana kati ya Kutekwa na Kukamatwa. 2.Kama walikuwa ni askari wa Jeshi la Polisi kweli walishindwa nini Kumuonyesha Kitambulisho mkamatwaji au majirani waliokuwa wanashuhudia. 3.Walishindwa nini Kuita gari ya Polisi wenye uniforms waweze kuondoka naye. 4.kwanini wasiwe na Uniforms wote,Kwanini wasiwe na gari ya Jeshi la Polisi,kwanini wasionyeshe kitambulisho.? 5.Nimepost kuwapa mfano halisi watu wanavyotekwa,ukitoa ushirikiano tu ndiyo nitoleee hiyo. USICHOTWE KIZEMBE
Boniface Jacob969,324 次观看 • 1 年前

UKISTAAJABU YA NAPE, UTAYAONA YA ULEGA....! Nimeshangazwa kushtushwa sana na sauti pamoja na picha mjongeo zinazo muhusu Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdallah Ulega zikitembea mitandaoni tangu Asubuhi ya leo. Cha kushangaza ni 1. Jinsi anavyo ongea kwa njia ya simu na mtu mwingine maneno mazito bila ya Kuwa na tahadhari au kutafakari nafasi yake katika Jamii kama kiongozi mkubwa wa serikali. 2 .Namna anavyo elezea kwa ustadi na kwa ufahari jinsi alivyotumia rushwa kushinda uchaguzi wa nafasi ya Ubunge jimbo la Mkuranga ndani ya CCM na Uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani,kinyume kabisa na maadili na sheria za nchi. 3.kwamba anajiapiza kuwa akishidwa Ubunge ktk Jimbo la Mkuranga ndani ya CCM na Uchaguzi mkuu,Mkuranga na Jimbo la Mkuranga,Pwani hapatotawalika kabisaaaaa. Je waziri Abdallah Ulega anataka kutufundisha na sisi wengine tunaoshindwa uchaguzi ktk nafasi mbalimbali tusiwe wajinga kwa kukubali kushindwa kiungwana bali tunatakiwa sehemu tunazoshindwa zisitawalike..? Tumemsikia 4. Je kwa mtindo huu na muendelezo wa wateule wa Rais kutoka hadharani kipindi hiki na kuongea kauli zinazo kinzana na katika na sheria za nchi juu ya haki ya watu kuchagua na Kuchaguliwa tutarajie uchaguzi wa huru na haki ktk serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu mwakani..? Ni majuzi tu tumetoka kusikia kauli za Waziri Mwingine Nape akiwa Mkoani Kagera akiongea juu ya kura kutoamua mshindi katika uchaguzi Sasa tuna Waziri mwingine anaye zungumza hadharani jinsi anavyotumia Rushwa na Ubabe katika Uchaguzi wa Mbunge jimboni kwake.
Boniface Jacob237,091 次观看 • 1 年前

POLISI WAWILI WAUA KWA MAAGIZO YA MKUU WA MKOA CHALAMILA. 1. Polisi wawili waua kwa risasi mlinzi wa Bar maarufu ya Boardroom iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam. 2. Mlinzi waliyeuwawa kwa risasi anaitwa Razak Anan mwenye umri wa miaka 29 muajiriwa wa Bar ya Boardroom, Sinza 3. Polisi kutoka kituo cha Polisi Mabatini walifika na gari na kupaki nje ya Bar ya Board room na kuanza msako wa Dada poa kwa kusema ni agizo la Mkuu wa Mkoa. 4. Lakini Polisi hao walikuwa wakiwatoa nje wahudumu na wateja katika Bar hiyo ambao walikuwa na min skirt (sketi fupi) kwa kusema kuwa watu hao kwa mavazi yao walikuwa wanajiuza katika Bar hiyo ya usiku (night Club) 5. Wateja wengine walipona udhalilishaji na manyanyaso hayo walianza kuondoka katika Bar hiyo ya Boardroom na waliobakia waligoma kutolewaa nje ya Bar kwa muonekano wa mavazi yao. 5. CCTV za Bar ya Board room inayonyesha Polisi hao walipoona wadada wanakata kufananishwa na machangudoa walienda katika gari na kuchujua silaha aina ya bunduki (SMG) na kuanza kutishia wateja na kuelekezea katika meza za wateja waliokuwa wanakunywa katika Bar hiyo. 6. Polisi hao ambao walikuwa wanaonekana wametumia kilevi walifyatua risasi kadhaa kisha kuondoka na gari yao kutoka eneo hilo la Bar ya Boardroom na baada ya kuondoka wateja walirejea na kukuta mlinzi mmoja wapo akiwa amelala chini akiwa amepigwa risasi na kuvuja damu nyingi (video inaonyesha damu ya marehemu) 7. Mlinzi wa Board room alifariki njiani akiwa katika Bajaji anakimbizwa hospitali. 8. Matukio ya polisi kuvamia sehemu za starehe na nyumba za watu binafsi ni maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye anaendesha zoezi la kutafuta madanguro na kusaka madada poa. 9. Leo Mkuu wa Mkoa amesisitiza mauaji kufanywa na polisi ni Jambo la kawaida "Mtu akifia kituo cha polisi tunasema Polisi wameua, Mtu akifia hospitali tunasema ni Mapenzi ya Mungu" RC-DSM, Chalamila 10. Nawakumbusha kulaani tukio lolote la Polisi kuua raia kwa kisingizio chochote kile, Leo kwa huyu kesho kwake. Video za chini zikionyesha polisi hao wanafyatulia watu risasi. Boniface Jacob - Ex Mayor
Boniface Jacob259,160 次观看 • 2 年前

Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara anusurika kupigwa makofi na Wananchi Jimboni kwake. Azomewa na Wananchi kama mwizi kwa umbali mrefu Wananchi watoa onyo asikanyage tena SIRARI Ukimya wake kuhusu mateso na mauaji ya Wananchi Wanaozunguka mgodi wa Nyamongo ndiyo chanzo. Wananchi wanajipanga kutafuta mtetezi na msemaji mwingine wa matatizo yao.
Boniface Jacob184,585 次观看 • 1 年前

😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭. Nilitegemea haya,nilipoona tumeshindwa kuperfome kama timu kwa miaka 4, Sasa kama hana cha kusema baada msimu kuisha afanyeje..? Lazima atajikuta anasemea CCM badala ya SIMBA Lazima tu timu ijishughulishe na vituko vya Kijinga kama hivi. Kwamba Msemaji wa timu hajui Simba ni mchanganyiko wa watu wenye vyama tofauti tofauti..? Nasikitika Kusema kuna uwezekano mkubwa mwaka huu tukagombea nafasi ya Pili au ya tatu tena.
Boniface Jacob151,160 次观看 • 1 年前

MUDA WA KAMPENI HUU😂😂😂😂 Wahuni wamemtegeshea chuma tupu,Mheshimiwa Mbunge akawa ana pump hewa 😂😂😂 Walipo kuja Kuondoa chuma cha kupamp bomba wakakuta chini hakuna kisima wala nini..! 😂😂😂 Vinaitwa Visima vya mwendo kasi. Nasikitika ndoto zake za Ubunge zilifutika hapo hapo 😂😂😂
Boniface Jacob92,697 次观看 • 1 年前

Leo imekuwa siku mbaya sana Kwangu na kampuni ya BONIYAI COMPANY LTD. Temepata mtihani na majaribu makubwa katika biashara na Ufugaji wetu tangu tuanze mwaka 2020. Ni hasara kubwa Kuvunjika Banda letu Jipya la "Boniyai layers poultry farming phase 2,Bagamoyo,mapinga,amani 1,ukubwa wa 20meters to 80meters". Ambalo Ujenzi ulikuwa ukamilike mwakani 2024,January na Kungiza batch ya kuku 40,000,CAGED Tumepoteza pesa,maarifa na muda ila hatujapoteza lengo,mikakati na dhamira. We shall stand again..! Ayubu 1:6 "BWANA akamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, kila kitu alicho nacho kiko mikononi mwako, lakini juu ya huyo mtu mwenyewe usimguse hata kwa kidole.”
Boniface Jacob180,188 次观看 • 2 年前

USHAHIDI WA VIDEO JINSI POLISI WALIVYOTEGEA MSAFARA WA FREEMAN MBOWE PORI LA HALUNGA-MBOZI 1.Baada ya mkutano wa Freeman Mbowe kuvurugwa na Jeshi la Polisi kupiga mabomu ya machozi mkutanoni eneo la Mlowo. 2.Freeman Mbowe na msafara wake waliamua kwenda eneo lingine kuendelea na kampeni za Vijiji. 3.Jeshi la Polisi walikuwa eneo la Mlowo wakati Freeman Mbowe ma wenzake wanaanza safari kwenda eneo lingine lakini hawakukamata. 4.Polisi walikwenda katika pori la Halungu kutegea msafara wa Freeman Mbowe ili wawapige na kuwadhalilisha 5.Polisi walifunga njia katikati ya pori la Halungu ambapo mtandao wa simu (Network) hakuna. 6.Wakamshusha Freeman Mbowe kwa nguvu kutoka katika gari kisha kutokomea naye kusikojulikana 7.Watu wengine waliokuwa katika msafara wa Freeman Mbowe walishushwa kwa nguvu na vipigo huku magari yakivunjwa vioo ili watolewe ndani 8.Vifaa vya waandishi wa habari na wapiga picha kama laptops na camera na microphone vikiporwa na Jeshi la polisi 9.Baadhi ya Viongozi na Wanahabari waliokamatwa katika tukio hili ni Sugu,Haonga,Appolo,Bwire,Maafisa habari Kanda ya Nyasa,Mdude 10.Wote kwa sasa wanashikiliwa kituo cha Polisi Vwawa. Boniface Jacob Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani.
Boniface Jacob106,929 次观看 • 1 年前

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha Godbless Lema na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha Boniyai. Tunaendelea kutunza kumbukumbu. Mpaka sasa Mkoa wa Arusha ndiyo wanashikilia rekodi ya kuchangia zaidi tonetone mkutanoni ,kiasi cha Tsh 1,335,000/= Leo mkoa wa Kilimanjaro, Moshi wameshika nafasi ya pili kwa kuchangia tonetone kiasi cha Tsh 1,095,000/= N.B T Kama kamati tumekubaliana kila mkutano tunamtumia M-Pesa msajili Mzee Francis Mutungi kiasi cha Tsh 30,000/= ya vocha aonje matunda ya tonetone kwa kusaidia kuhamasisha wananchi kutuchangia mikutanoni. Asanteni sana
Boniface Jacob74,600 次观看 • 1 年前

POLISI YAUA TENA IRINGA Mwanamke mmoja katika Manispaa ya Iringa amepoteza maisha baada ya kupokea kichapo kutoka Jeshi la Polisi. Polisi wakiwa katika zoezi la kuondoa wafanyabiashara ndogondogo katika Manispaa ya Iringa. Polisi walikuwa wanatumia nguvu kuwakata na kuwapiga baadhi ya wakina mama waliokuwa wanauza mboga na kutembeza ndizi eneo la mashine 3-Iringa. Mwanamke huyo ambaye bado natafuta jina lake na ndugu zake kupita uongozi wa wafanya biashara amefariki baada ya kupigwa na Polisi hadi presha kushuka. Video inaonyesha wakina mama wenzie wauza mbogamboga wakimpatia Mwanamke huyo huduma ya kwanza, muda mchache baada ya kupoteza fahamu na baadae kuaga Dunia. Nawapa pole sana wakina mama wote ambao ni wapambanaji wa maisha kwa kupitia biashara ndogondogo. Najua mlijua Rais akiwa Mwanamke mwenzenu huenda anajua shida zenu zaidi. Poleni.
Boniface Jacob146,209 次观看 • 2 年前

Mchuma umekutwa maeneo ya Gongolamboto ukiwa UMEKATA PUMZI. Wasamaria wema wanasema UMEME UMEKATIKA na halina Chaji. Wengine wanasema LIMECHOKA kutembezwa ovyo LIMEZIMIKA lipumzike.😂😂😂 Mafundi wameshafika eneo la tukio,wanalibembeleza liamke liendelee na safari. Limeomba MO ENERGY kwanza.
Boniface Jacob119,569 次观看 • 2 年前

Kama hapo ni AIRPORT yetu ya KIMATAIFA Gari inateketea mbele ya Zimamoto pamoja na Kuwa ndiyo sehemu yenye Gari za Zimamoto Kuliko sehemu yoyote. Vipi Kuhusu Mimi na Wewe wa Kilungule,Saranga,Matosa,Kibesa au Tandale kwa Mkunduge Au kiitwe KIKOSI CHA KUCHOCHEA MOTO......?
Boniface Jacob142,365 次观看 • 2 年前

JESHI LA POLISI MNAPEWA NINI NA FAMILIA YA GEKUL...? Inawezekanaje mdogo wa Pauline Gekul nayeitwa EMMANUEL FILIPO GEKUL Akapigia simu wati wote waliopost na kusambaza habari kuhusu Dada yake PAULINE GEKUL alipokuwa Naibu waziri kumtesa na kumdhalilisha kijana Ally Hashimu kuwa atawapiga risasi na kuwakata Vichwa...? Polisi mpo mnaangalia tu..? Kwenye Sauti ni EMMANUEL FILIPO GEKUL akiwa anasema kuwa ata muua kwa Kumkata kichwa au Kumpiga risasi PAULINA SLAA NARSIS. Dada Paulina Slaa Narsis ameshatoa toa taarifa ktk Jeshi la Polisi Babati,lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na Jeshi la Polisi hadi dakika hii. Wananchi wa mkoa wa Manyara na wilaya ya Babati wanataka kujua familia ya Pauline Gekul kama iko juu ya sheria..? RPC,RCO,OCD,OC-CID wa Manyara na Babati wanapewa nini kutoka ktk familia ya Pauline Gekul.....? Je wanapata wapi kiburi na Jeuri ya Kufanya Jinai kwa Kupiga simu kutishia kuua watu..? Vipi Bwana EMMANUEL FILIPO GEKUL akaua kweli hapo Babati,Mtatuambia mlikuwa hamjui .? Ndiyo maana Jana nilisema Jeshi la Polisi Manyara na Babati lichunguzwe na washirika wa Pauline Gekul wawajibishwe haraka sana...!
Boniface Jacob133,154 次观看 • 2 年前