
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema • 1,250,277 subscribers
Politician/Activist/Member @Chadematz Member of Central Committee , Former MP Arusha Urban (2010 -2020), Shadow Minister Home Affairs, Husband and Father
Shorts
Videos
0:44
Sensitive content
This media may contain sensitive content.

Hakustahili huu unyama hata kidogo. Ukosoaji wake na utoaji wa maoni ni wa kawaida. Lakini kapigwa na kudhalilishwa kwa kiwango hiki. Kuna hasira kali sana ndani yake. Amekubali na kuridhia kupigwa picha na kuirusha huku sehemu zake za siri (matako) zikiwa uchi? Tipping point. Hii hasira ni pando linalopanda kisasi kwa jamii yote katika siku si nyingi? Kila mtu atapoteza amani na furaha. Wakati utasema. Nani kafanya unyama huu? Kundi gani? Kwa manufaa gani? Na nani anafuata? Na maumivu haya yanaweza kuvumiliwa mpaka lini? Haya ni maswali ya msingi ya kujiuliza, hasa zaidi wana CCM.
Godbless E.J. Lema64,154 views • 26 days ago

Huu Upumbavu na Ubaguzi Unapaswa Kushugulikiwa Kikamilifu Sana.
Godbless E.J. Lema232,269 views • 1 year ago

Nina wasiwasi. Huyu mtuhumiwa anaonekana very smart, strategic na sharp. Lakini namna anavyoomba msamaha mbele ya RC… mmmh. Naguna kabisa. Pengine hakuna sinema yoyote; labda tu nimeathiriwa na movies za CIA na Mossad ambazo nimekuwa nikiziangalia sana. Maana mara nyingine unaanza kuona patterns, narratives na hidden motives kila mahali. Lakini bado, kuna kitu hakikai sawa. Mtu ambaye anaonekana composed na calculated, ghafla awe mnyenyekevu kiasi hicho mbele ya mamlaka , naturally inafanya watu waulize maswali, Je, ni hofu ya kawaida? Ni pressure? Ni survival instinct? Au kuna narrative fulani inatengenezwa? Sina majibu. Nauliza tu.
Godbless E.J. Lema60,544 views • 4 months ago

Sikutilia maanani sana hizi video mwanzoni. Lakini nilianza kuziangalia kwa uzito zaidi pale nilipogundua kuwa maudhui ktk video hii yaliwekwa kwenye ukurasa wa Instagram wa gazeti la Habari Leo, gazeti la serikali, na baadaye yakaondolewa. Na haya ni maneno ya Makamu wenu wa Rais. Kinachonishangaza ni kwamba maudhui yaliyomo yanalenga kukemea ufisadi wa fedha za umma na viongozi kuacha kujinufaisha. Swali la msingi linaanzia hapa, kama maneno ya aina hii yanaweza kuonekana mabaya kiasi cha kuondolewa, basi wale wananchi wote wenye akili na mapenzi ya nchi wanapaswa kujiuliza kwa kina mwelekeo wa zaidi tunaokwenda. Je, ni rahisi kwa mhariri kuamua kuondoa maudhui yanayomhusu kiongozi wenu wa juu namna hiyo bila maelekezo kutoka juu? Na huko juu ni wapi ? Kuna hadithi moja huko Italia , askari wa barabarani alisimamisha gari , alipokuwa anakagua, akagundua kuwa aliyekuwa anaendesha alikuwa PAPA , ghafla alianza kukimbia kwa speed kali huku akitokwa jasho !! Wenzake walimuona na kumfuata na kumuuliza , nini kimekupata ? Alijibu , nimesimamisha gari nikakuta PAPA anaendesha akiwa na abiria mmoja , akaendelea kusema , nafikiri huyo abiria lazima atakuwa YESU !! Tafakari. Huyu ni Makamu wa Rais wa serikali yenu mliyopata kupitia uchaguzi uliokuwa na maumivu makubwa kwa taifa. Mnaondoa video kama hii ktk kurasa zenu, meseji kwa umma ni moja , Amkeni sasa na sio baadae, maana Cartels wako RADA. Nina hofu kuhusu kesho ya Tanzania. Si kwa sababu hakuna watu wenye uwezo, bali kwa sababu ukimya unapokuwa kawaida, hata mambo yasiyostahili yanaendelea kuonekana ya kawaida. Hapo ndipo hatari kubwa. CCM, mnapaswa kutafakari kwa kina. Historia ina tabia ya kurudia matokeo yake pale pale makosa yanapopuuzwa. Hii si wakati wa kiburi, bali ni wakati wa kurekebisha mwelekeo kwa ajili ya taifa. Kila maumivu mliyowapatia wa Tanzania , mtalipa na Nchi itaharibika sana. Maisha ya Nchi sio ushabiki wa michezo.
Godbless E.J. Lema63,306 views • 4 months ago

Simai , huko wapi Bro , kuna Chalii ananiparamia huku !!!
Godbless E.J. Lema40,922 views • 3 months ago

Mh Rais Nakusalimu. Tumetoka Mwananyamala Hospital , Majeruhi Rafiki Zetu Na Viongozi Wenzetu Ambao Tumewakuta Wako Tisa (9) Waliokamatwa Leo Mahakamani , Lakini Yuko Mtu Mmoja Tumeambiwa Alipigwa Sana Na Tunaambiwa Amekufa, Tumefika Mochwari Tukakuta Polisi Wanataka Kushusha Maiti. Tulikaa Pembeni Ili Wamalize Kazi Yao , Badala ya Mwili Kushushwa Ili Tuweze Kuitambua Hiyo Maiti, Badala Yake Gari Ya Polisi Ilikimbia Na Kuondoka na Mwili Wa Marehemu Wkt Tulikuta Marehemu Alikuwa Amekwisha Andikishwa Kuingia Mochwari. Nimesema Nikupe Taarifa Na Pia Nikutakia Kazi Njema Sana Na Mungu Akulinde Wewe Na Familia Yako. DAMU ITANENA.
Godbless E.J. Lema167,056 views • 1 year ago

Siku moja niliona umeandika mtandaoni kuwa unachukizwa sana na watu wanaoisema familia yako vibaya, hususani ulivyokuwa uki-post picha ya mtoto wako huku watu wakikejeli kuwa mtoto wako ameshiba kodi zetu. Sasa, Mwigulu, ulishawahi ku-imagine namna, mke au watoto wa Ally Kibao huwa wanajisikia baada ya baba yao kuuwawa kikatili ? Au Ben Saanane au familia ya Msafiri Mbwambo aliyeuwawa kwa kuchinjwa kwa chain saw wkt ule wa uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki wewe ulipokuwa unaratibu kampeni za CCM ? Mna mchapa mtu halafu akilia, mna mchapa tena kwa nini analia ? Very Narcissist personality. Chama chenu kimejenga chuki kubwa sana ktk jamii. Hata tofauti ya watu safi na wabaya ndani yenu haionekani tena hata kama wamo. Na hatari yake kila mtu anavuna kejeli ya collective responsibility. Pigeni U Turn Acheni Kiburi ! Mnashangaa watu kufurahia matatizo yenu lakini hamhuzunishwi na watu wanaopotea na kufa bila miili hata miili yao kupatikana ? Mnafikiri nyie mnapaswa kuishi kwa starehe tu lakini the rest waishi maisha ya wasiwasi ? Anyway, unakumbuka mjadala wangu Mimi na wewe wkt ule ukiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mimi Waziri Kivuli kuhusu mawuaji na utekaji ? Leo nitaishia hapa. Pigeni U Turn Acheni Kiburi. Mmeumiza sana watu na Nchi , mateso yamegeuka hasira na hasira imeumba chuki. Kuna njia mbele ya kutoka hapa , nayo ni HAKI.
Godbless E.J. Lema64,352 views • 5 months ago

Huu sio uwekezaji hata kidogo. Nilisema hapo nyuma na ninarudia tena hapa Coco Beach panahitaji brain power. Ni ufukwe bora kabisa katika Jiji la Dar es Salaam na mipango yake haiwezi kuendeshwa kwa mjadala uliobeba poverty mentality. Jitihada yoyote ya kurekebisha Coco Beach ili kubeba quality standard mimi nitakuwa mshirika wake ktk jitihada hizo. Nafurahi kwamba ukweli ktk eneo hili umeanza kusikika. Mindset transformation is bigger than voting collection.
Godbless E.J. Lema58,018 views • 5 months ago

Hii inaitwa Red Herring , mkakati wa kuingiza hoja ya pembeni ili watu waache mada kuu na jambo la msingi katika jamii. Wakati mwingine huitwa pia manufacturing consent , kutengeneza jambo kwa umma kwa njia ya udhibiti wa taarifa muhimu. Kwa lugha rahisi, ni mkakati wa kuhamisha umakini wa watu kutoka kwenye suala nyeti kwenda kwenye jambo lingine (mara nyingi la hisia, burudani au mgogoro) ili kupunguza shinikizo, uchunguzi na mjadala.
Godbless E.J. Lema50,650 views • 5 months ago

Hii ni kauli mbaya sana. Nafikiri kuna tatizo kubwa sana. Nasikitika kuwa imetolewa na Kiongozi kutoka ktk Chama changu. Nashindwa kupuuza maneno haya kwa namna yoyote ile. Maneno haya yanajengwa na mikakati wa siri ambayo wengi tunanaweza kuwa tunaiona lakini tunaogopa kuchukua hatua. Siasa zenye misingi ya udini sio za bahati mbaya ktk Nchi hii. Kauli chafu kabisa hii wala sio ya bahati mbaya. Siri zikiwa nyingi moyoni huwa zinatoka zenyewe.
Godbless E.J. Lema172,776 views • 1 year ago

Kitu gani hiki ? Na serikali iko kimya ? Kwamba mtu haruhusiwi kula Zanzibar wkt wa mfungo wa mwezi Ramadhan ? Na sauti inasikika ikisema kuwa hapa sio Bara !!! Haya mambo sio madogo hata kidogo,yana chochea chuki ktk jamii haijalishi anayetendewa ni nani na wa dini gani.Hii ni hatari kubwa sana.Anyway Mama anaupiga mwingi.
Godbless E.J. Lema202,721 views • 2 years ago