
Godbless E.J. Lema
@godbless_lema • 1,247,191 subscribers
Politician/Activist/Member @Chadematz Member of Central Committee , Former MP Arusha Urban (2010 -2020), Shadow Minister Home Affairs, Husband and Father
Shorts
Videos

Nina wasiwasi. Huyu mtuhumiwa anaonekana very smart, strategic na sharp. Lakini namna anavyoomba msamaha mbele ya RC… mmmh. Naguna kabisa. Pengine hakuna sinema yoyote; labda tu nimeathiriwa na movies za CIA na Mossad ambazo nimekuwa nikiziangalia sana. Maana mara nyingine unaanza kuona patterns, narratives na hidden motives kila mahali. Lakini bado, kuna kitu hakikai sawa. Mtu ambaye anaonekana composed na calculated, ghafla awe mnyenyekevu kiasi hicho mbele ya mamlaka , naturally inafanya watu waulize maswali, Je, ni hofu ya kawaida? Ni pressure? Ni survival instinct? Au kuna narrative fulani inatengenezwa? Sina majibu. Nauliza tu.
Godbless E.J. Lema60,347 просмотров • 28 дней назад

Sikutilia maanani sana hizi video mwanzoni. Lakini nilianza kuziangalia kwa uzito zaidi pale nilipogundua kuwa maudhui ktk video hii yaliwekwa kwenye ukurasa wa Instagram wa gazeti la Habari Leo, gazeti la serikali, na baadaye yakaondolewa. Na haya ni maneno ya Makamu wenu wa Rais. Kinachonishangaza ni kwamba maudhui yaliyomo yanalenga kukemea ufisadi wa fedha za umma na viongozi kuacha kujinufaisha. Swali la msingi linaanzia hapa, kama maneno ya aina hii yanaweza kuonekana mabaya kiasi cha kuondolewa, basi wale wananchi wote wenye akili na mapenzi ya nchi wanapaswa kujiuliza kwa kina mwelekeo wa zaidi tunaokwenda. Je, ni rahisi kwa mhariri kuamua kuondoa maudhui yanayomhusu kiongozi wenu wa juu namna hiyo bila maelekezo kutoka juu? Na huko juu ni wapi ? Kuna hadithi moja huko Italia , askari wa barabarani alisimamisha gari , alipokuwa anakagua, akagundua kuwa aliyekuwa anaendesha alikuwa PAPA , ghafla alianza kukimbia kwa speed kali huku akitokwa jasho !! Wenzake walimuona na kumfuata na kumuuliza , nini kimekupata ? Alijibu , nimesimamisha gari nikakuta PAPA anaendesha akiwa na abiria mmoja , akaendelea kusema , nafikiri huyo abiria lazima atakuwa YESU !! Tafakari. Huyu ni Makamu wa Rais wa serikali yenu mliyopata kupitia uchaguzi uliokuwa na maumivu makubwa kwa taifa. Mnaondoa video kama hii ktk kurasa zenu, meseji kwa umma ni moja , Amkeni sasa na sio baadae, maana Cartels wako RADA. Nina hofu kuhusu kesho ya Tanzania. Si kwa sababu hakuna watu wenye uwezo, bali kwa sababu ukimya unapokuwa kawaida, hata mambo yasiyostahili yanaendelea kuonekana ya kawaida. Hapo ndipo hatari kubwa. CCM, mnapaswa kutafakari kwa kina. Historia ina tabia ya kurudia matokeo yake pale pale makosa yanapopuuzwa. Hii si wakati wa kiburi, bali ni wakati wa kurekebisha mwelekeo kwa ajili ya taifa. Kila maumivu mliyowapatia wa Tanzania , mtalipa na Nchi itaharibika sana. Maisha ya Nchi sio ushabiki wa michezo.
Godbless E.J. Lema62,862 просмотров • 1 месяц назад

Siku moja niliona umeandika mtandaoni kuwa unachukizwa sana na watu wanaoisema familia yako vibaya, hususani ulivyokuwa uki-post picha ya mtoto wako huku watu wakikejeli kuwa mtoto wako ameshiba kodi zetu. Sasa, Mwigulu, ulishawahi ku-imagine namna, mke au watoto wa Ally Kibao huwa wanajisikia baada ya baba yao kuuwawa kikatili ? Au Ben Saanane au familia ya Msafiri Mbwambo aliyeuwawa kwa kuchinjwa kwa chain saw wkt ule wa uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki wewe ulipokuwa unaratibu kampeni za CCM ? Mna mchapa mtu halafu akilia, mna mchapa tena kwa nini analia ? Very Narcissist personality. Chama chenu kimejenga chuki kubwa sana ktk jamii. Hata tofauti ya watu safi na wabaya ndani yenu haionekani tena hata kama wamo. Na hatari yake kila mtu anavuna kejeli ya collective responsibility. Pigeni U Turn Acheni Kiburi ! Mnashangaa watu kufurahia matatizo yenu lakini hamhuzunishwi na watu wanaopotea na kufa bila miili hata miili yao kupatikana ? Mnafikiri nyie mnapaswa kuishi kwa starehe tu lakini the rest waishi maisha ya wasiwasi ? Anyway, unakumbuka mjadala wangu Mimi na wewe wkt ule ukiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mimi Waziri Kivuli kuhusu mawuaji na utekaji ? Leo nitaishia hapa. Pigeni U Turn Acheni Kiburi. Mmeumiza sana watu na Nchi , mateso yamegeuka hasira na hasira imeumba chuki. Kuna njia mbele ya kutoka hapa , nayo ni HAKI.
Godbless E.J. Lema64,081 просмотров • 2 месяцев назад

Huu sio uwekezaji hata kidogo. Nilisema hapo nyuma na ninarudia tena hapa Coco Beach panahitaji brain power. Ni ufukwe bora kabisa katika Jiji la Dar es Salaam na mipango yake haiwezi kuendeshwa kwa mjadala uliobeba poverty mentality. Jitihada yoyote ya kurekebisha Coco Beach ili kubeba quality standard mimi nitakuwa mshirika wake ktk jitihada hizo. Nafurahi kwamba ukweli ktk eneo hili umeanza kusikika. Mindset transformation is bigger than voting collection.
Godbless E.J. Lema57,923 просмотров • 2 месяцев назад

Hii inaitwa Red Herring , mkakati wa kuingiza hoja ya pembeni ili watu waache mada kuu na jambo la msingi katika jamii. Wakati mwingine huitwa pia manufacturing consent , kutengeneza jambo kwa umma kwa njia ya udhibiti wa taarifa muhimu. Kwa lugha rahisi, ni mkakati wa kuhamisha umakini wa watu kutoka kwenye suala nyeti kwenda kwenye jambo lingine (mara nyingi la hisia, burudani au mgogoro) ili kupunguza shinikizo, uchunguzi na mjadala.
Godbless E.J. Lema50,547 просмотров • 2 месяцев назад

Wapumbavu wakipeana sifa, upumbavu hugeuka huduma. Wasio na utambuzi hupiga makofi wakidhani ni baraka. Kelele zinapozidi bila maana, ujue si hekima inayoongea, ni ujinga uliopata jukwaa. Tatizo si mavazi wala vipaza sauti, bali ujumbe usio na maarifa unaopotosha jamii. Kikao hiki kimekutanisha upumbavu na ushamba. Kundi la wapumbavu likiongozwa na upumbavu, mwisho wake ni aibu. Angalia na sikiliza huu UPUMBAVU wa huyu content creator.
Godbless E.J. Lema48,302 просмотров • 2 месяцев назад

Huu Upumbavu na Ubaguzi Unapaswa Kushugulikiwa Kikamilifu Sana.
Godbless E.J. Lema232,211 просмотров • 1 год назад

Usafiri wa boda boda(Pikipiki) haukupaswa kuwa usafiri wa umma. Boda boda imegeuka njia ya kupeleka vijana na watu wengi kwenye vifo, ulemavu na umasikini. Ukosefu wa sera za uchumi, usalama barabarani, na ujinga wa kisiasa ni msingi mkuu wa janga hili. Kutega kura kwa gharama ya damu ni dhambi na ujinga wa kiwango cha juu. Kukaa kimya ni kushiriki kwenye mauaji na mateso haya. Vijana hawa siku moja, watashituka kuwa hawakuongozwa vyema na hali itakuwa mbaya sana kwenu.
Godbless E.J. Lema39,702 просмотров • 2 месяцев назад

Mh Rais Nakusalimu. Tumetoka Mwananyamala Hospital , Majeruhi Rafiki Zetu Na Viongozi Wenzetu Ambao Tumewakuta Wako Tisa (9) Waliokamatwa Leo Mahakamani , Lakini Yuko Mtu Mmoja Tumeambiwa Alipigwa Sana Na Tunaambiwa Amekufa, Tumefika Mochwari Tukakuta Polisi Wanataka Kushusha Maiti. Tulikaa Pembeni Ili Wamalize Kazi Yao , Badala ya Mwili Kushushwa Ili Tuweze Kuitambua Hiyo Maiti, Badala Yake Gari Ya Polisi Ilikimbia Na Kuondoka na Mwili Wa Marehemu Wkt Tulikuta Marehemu Alikuwa Amekwisha Andikishwa Kuingia Mochwari. Nimesema Nikupe Taarifa Na Pia Nikutakia Kazi Njema Sana Na Mungu Akulinde Wewe Na Familia Yako. DAMU ITANENA.
Godbless E.J. Lema166,973 просмотров • 1 год назад

Huu ni upotoshaji. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba rangi hizi zinawakilisha LGBTQ+. Hizi ni rangi za kawaida zinazotumika kila siku katika elimu, sanaa na ubunifu. Kuzihusisha moja kwa moja na ajenda fulani bila msingi ni uoga usio na sababu na tafsiri ya haraka isiyo na uthibitisho. Rangi za LGBTQ+ zina utambulisho wake maalum kupitia rainbow flag yenye mpangilio unaojulikana: red, orange, yellow, green, blue na purple. Kama nilivyoonyesha ktk picha hapa. Hizi unazoona ni ubunifu wa kawaida kabisa kama rangi za watoto au michoro ya kijamii. Kinachokera zaidi ni kuona imani ya Kikristo ikidhalilishwa kwa maamuzi ya haraka yasiyo na mantiki. Kuzuia mkutano wa injili kwa sababu ya rangi ni kuonesha udhaifu wa kufikiri na kuipa hofu nafasi ya kuongoza badala ya ukweli. Tuache kudhoofisha na kudhalilisha imani yetu kwa maamuzi ya papara. Imani ya Kikristo haihitaji kulindwa kwa hofu wala kwa kuchanganya mambo yasiyo na uhusiano. Inahitaji kusimamiwa kwa ukweli, ujasiri na hekima. Serikali imefanya udhalilishaji mkubwa dhidi ya imani ya KIKRISTO , na kwa viongozi wa dini maamuzi ya kuomba radhi bila kuchambua kwa kina yanaweza kuleta picha ya kukosa msimamo na kuendelea zaidi kudhalilisha Kanisa. Kanisa lina wajibu wa kusimama imara katika ukweli, si kuyumbishwa na tafsiri zisizo na msingi. Kazi ya Kanisa si kuogopa vivuli, bali kusimama katika nuru ya kweli. Kupambana na uovu hakumaanishi kupoteza mantiki.
Godbless E.J. Lema38,317 просмотров • 2 месяцев назад

Kupigania haki na demokrasia kunahitaji kuheshimu na kupenda dhamira yako zaidi kuliko kuangalia watu unao wapigania, vinginevyo sababu za kukata tamaa zinaweza kuwa wazi. Imagine mtu anajivunia kwa ufasaha uhalifu ndani ya chama chake, halafu watu walioko mbele yake wanashangalia. Ni muhimu sana kama jamii, kuwa wakati tunaongea kuhusu uhitaji wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ni muhimu pia kuelewa tunahitaji mindset transformation ya hali ya juu, haswa kuanzia ktk level ya familia. Hakuna kinachoweza kujenga ustawi wa nchi bila kubadilisha fikra hasi na mbaya zilizoishika jamii na bahati mbaya zimekuwa normalized kama kanuni za kawaida za maisha. Tuna hatari kubwa sana.
Godbless E.J. Lema39,998 просмотров • 2 месяцев назад