正在加载视频...

视频加载失败

Ruvuma ya Mama ❤️

131,586 次观看 • 1 年前 •via X (Twitter)

0 条评论

暂无评论

原始帖子的评论将显示在这里

相关视频

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Ndugu Oddo Mwisho, amesema CCM haijakurupuka kufanya maamuzi ya kumfukuza uanachama aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, na kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, hana mgogoro na Dkt. Nchimbi. Amesema mwanachama yeyote anayekiuka taratibu za chama, chama kina uwezo wa kuchukua hatua dhidi yake bila kujali nafasi yake. Akizungumza na wananchi wa kata za Langiro, Kipapa na Maguu zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama tarehe 31/8/2026, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma, Ndugu Oddo Mwisho, amesema Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ni mwana wa Ruvuma na ni ndugu yao. Amesema Mkoa wa Ruvuma ulikuwa unamtegemea kutokana na nafasi aliyokuwa nayo ya Makamu wa Rais, lakini amewaangusha wananchi wa Ruvuma kwa bahati ambayo Rais Samia aliipa mkoa huo kwa kumchagua mmoja wa vijana wa mkoa huo kuwa msaidizi wake namba moja. Katika hatua nyingine, Ndugu Oddo Mwisho amemuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkt wa CCM ,Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa changamoto iliyotokea. Amesema yaliyofanywa na Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ni ya kwake binafsi na si ya wananchi wa Ruvuma, kwani wananchi wa Ruvuma wana imani na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye bado anawaamini vijana Mbalimbali walioko ndani ya Mkoa huo ambao wanafanya kazi vyema katika Chama na serikali.

Royal Media

18,567 次观看 • 10 天前